Sultana Written Updates Tuesday May 9 2023

Becky

Posted by kiongos on 2023-05-09 12:59:31 |

Share: Facebook | Twitter | Whatsapp | Linkedin Visits: 846


Sultana Written Updates Tuesday May 9 2023

Sultana Written Updates 

Tuesday May 9 2023


Major ashatokwa na JJ na ndio huyu anarudi nyumbani anapiga mguu. Akiwa barabarani mawazo si mawzo,juzi tu amekua sonko,sai sasa yeye na ile panya ya church tofauti ni mkia tu. Kumbe Major alitaka JJ na Sultana wakuje ndio Sada amhurumie ju anajua Sada huwa na soft heart ikifika kwa Sultana na JJ but sasa JJ ashaambia Major asiwa,na asiwai dhubutu kumpigia wala kumtafuta. Hii shida ya Major imeletwa na nani? Fatima,baaasi Major ashajua hilo an sasa kama kuna mtu anaenda kuhakikisha anmuondokea ni Fatima.Hivi ndio Major anasema akitembea. Imagine juzi tu amekua millionaire sai bank acount zake zoote 15 zimekua freezed na Sada😢😢


JJ na Sultana walikuja out,wakajionea wanyama,akina Girraffe,akina nyani,akina ngurue,akina Pauloh,yani wamekuja kwenye mbuga ya wanyama na hii ni raha sana kwa Sultana hususani akiwa na JJ kando yake. Mnaona venye Sultana anafeel,hivi ndio Xtine hufeel akiwa na mimi😂😂😂JJ anamuahidi Sultana atafanya juu chini apate kuona tena.


Dida baada ya kuwaza na kuwazua,alikuja kumuomba babake msamaha kwa kumuongelesha vile ile masaa,lakini babake alimwambia you know what my daughter,you were right and I ant blame you. Dida akamuuliza so umeamua aje,tunahama ama we remaining here? Buya hakumjibu lakini akienda alismile,anaenda wapi? Kuleta chupa ya champaigne🥰🥰🥰kwa wale hamjui kazi ya champaign hutumika kusherehekea furaha na maisha mazurimsi hata pia unaona nyinyi hamjai kunywa champaigne,now you know why! Dida na babake wana futaa kwanza washamtoa Fatima kwa maisha yao even though she is on lose.


JJ ba Sultana baada ya kuona wanyama,walikuja sasa ufuoni mwa bahari,wakafurahi,wakabebana,wakakimbia huku wakichezea chezea maji wakiwa na furaha sana. Baadaye walishika njia kurudi nyumbani na wanatembea kama wameshikana tu,huku Sultana anasema anaimagine tu wakati ataweza kuona kisha amuon Major ambaye kwanza ni adui wake mkubwa na pili ni babake mzazi. JJ alimwambia kuhusiana na Major usiwe na wasiwasi kwa sababu hataweza kwa namna kuja kukutafuta ama kukujerui,Sultana akamuuliza una uhakika gani ama jana ukitoka asubuhi ulienda kuonana na yeye? JJ akamwambia ndio,nilienda nikamuona na nikampasha.


Tufike kwa mama yetu Sada,alimuita Mwanzele akauliza,huyu Major uliema alitoka akaenda joging,mbona hajarudi ama ulikua unanitania? Mwanzee akamwambia madam,ametoka hapa akiwa amevalia magwanda yake na akaenda joging na kama unataka kujua kwenye ameenda,chukua simu yake uangalia watu ameongea nao. Sada akamwambia Mwanzele sikiza,wewe ni mtu mzima,mbona uliamini kuwa Zuu alikufa kwa kuumwa na nyoka na ukakataa kumsikzia Kaka? Sada alimwambia Mwanzele,Kaka alikua na maoni tofauti sana na ungempa nafasi umsikize,ungejua nini kilimuua bibi yako but ju ya ujinga wako hukumsikiza,hata ondoka hapa! Kunguni!


Maria alikuja kuuliza Asiya ilikuaje ukakuja ikafika unafanya kwai kwa Major? Asiya hakumjibu. Maria akamwambia kulingana na venye nimekuona,hukao mtu wa mangori,lazima kuna mtu alikuroundia kama venye mimi nilifanyiwa hadi sai namiss Kanairo,namiss bae wangu Luwi na hata maybe sai tungekua na katoto ketu. Wakati Maria alisema katoto,akakumbuka wait,kuna kitu hafai kuacha nyumba akatoka mbio kuenda kuangalia.


Kwa Salama ishafika saa kumi na mbili na bado JJ na Sultana hawajafika na walikua na wasiwasi hawa watoto wako wapi,lakini punde si punde,wakafika. Ua akawauliza mbona mnaenda mbali na boma,ni hatari. JJ akawaambia msijali,nilienda nikaongea na Major na nikamhakikishia asidhubutu kufanya lolote so we are safe msiwe na shaka.


Asiya na yeye akiwa jikoni,Fatima alifika,akamuuliza,mbona uliambia Major ni mimi niliambia Sada yeye alimuua babake? Asiya akamwambia mimi sijaambia Major lolote Fatima. Fatima akamwambia haya,ili uwe salama,niambie Sada anapanga nini na ile will ameiweka nini. Asiya alimwambia yeye hajui na hajui kabisa. Fatima akamshika Asiya tai akitaka kumtandika na achunge sana,Maria anarudi.


Dida akiwa an babake alimuuliza babake kuhusu Sarah,maybe babake amuoe lakini Buya akamwambia usijali,hata kama unasema kweli,si haraka kwa sasa,kila kitu kinaenda pole pole na kwa wakati wake.


Maria akiwa kwa room akiangalia kama pete yake ilikua packect,alisikia jikoni kuna kelele ya Asiya akiambia Fatima niachilie. Maria akaweka pete kisha akatoka kuja jikoni. Huku jikoni,Fatima amekataa kuachilia Asiya na Asiya anaambia Fatima kama unataka kuuliza Sada maswali enda umuulize yeye mwenyewe,lakini punde si punde, Maria na Sada wakafika. Maria akamtoa Fatima mkono na akamwambia kama unataka vita,then pigana na mimi achana na Asiya. Fatima akamwambia Maria wee pia usiingilie hii,huyu si Buya na kwa taarifa yako,Buya ni zilizopendwa,we are officially divorced.


JJ na yeye akiwa amekaa,alikumbuka kuna kitu ilikua aambiwe jana na hawa wanawake wawili,Ua na Salama,hadi akawauliza nyie,mna uhakika hakuna jambo yafaa mniambie? Ua alitaka yeah yafaa tukuambie but Salama akakatiza akasema hamna,tuko sawa na pengine kukushukuru tu. Ua akaona zii,akaambia JJ kama swali,ukijua sasa hivi kuwa watu wako wako uhai utafanya aje? JJ akaambia Ua,mimi hilo jambo sitaki kusikia kabisa,mara ya mwisho nilipojaribu kujua chimbuko la familia yangu,ilikaribia nimuue mtu so hiyo story ya ooh familia yangu sijui iko wapi,mimi sitaki. Salama akafurahi.


Kumbe Major alifika akapata Fatima,Sada,Maria na Asiya akauliza kuna nini? Fatima akamwambia babe,imagine hawa watatu waliniita hapa wakataka kinichapa. Major akamwambia Fatima watu si wajinga,kwanza nataka uniambie barua ya Sultana uliificha kwa nini? Fatima akajifanya hajui,akasema barua gani sasa? Major akamwambia barua ya upasuaji wa Sultana,mbona uliificha? Fatima akamwambia hiyi hata haikua ya maana ama ulitaka ujue ndio iwe nini...hata Fatima hakupewa nafasi ya kumalia kuongea,aliwekelewa kofi na Major,karibu aanguke. Wueh! Major ameamua sasa story za Fatima ni past tense. Sada alicheka hadi nikaacha kuandikia hapo😂😂siku ya kesho,majaliwa.

Watch Videos
Search
Search
Recent Updates