Sultana Written Updates Thursday May 11 2023

Becky

Posted by kiongos on 2023-05-10 21:23:26 |

Share: Facebook | Twitter | Whatsapp | Linkedin Visits: 661


Sultana Written Updates Thursday May 11 2023

Sultana Written Updates

Thursday May 11 2023


Major aliambia Fatima,hamna haja ya kumtoa  roho mtu,ima awe Sultana ama Sada,hakuna haja kuumiza mtu. Fatima alimwambia hizi ni vita,na vita havichagui  su hujiulizi mbona sikuhizi Sada anatushinda kwa kila jambo,ni kwa sababu habagui vita na habagui yeyote,so we should be doing the same. Major alimwambia ni sawa,itabidi nifikirie kwanza. Major alitoka nje,akapata Mwanzele amekaa hapo amehurumisha  na kusonona,  Major alimuita akamuuliza kwema?


Mwanzele akamwambia Major,wewe huwa wanionaje mimi? Huwa unaniona mjinga tu au mtu alielaaniwa sio? Major akamuuliza mbona useme hivi Mwanzele? Mwanzele akamwambia,mimi naamini mke wangu alikufa kwa kuumwa na nyoka lakini watu hawaoni hilo,wanaona mke wangu alikufa kwa kuumizwa na ndio maana Kaka amejitenga na mimi. Major akamuuliza,ni nani huyu amekupea hizi taarifa ati mke wako aliuliwa? Mwanzele akamwambia ni Sada. Major akaambia Mwanzele sikiza,huyu Sada usimsikize hata kidogo na usipochunga atakuja akuambie ni mimi niliua mke wako. Mwanzele akauliza Major niambie tu ukweli,umehusika kwa kifo cha mke wangu? Major akamwambia laah hasha,hamna kitu kama hilo na wewe enda ulale akili ipumzike.


Kumbe Fatima aliskia,akakuja akaambia Major unaona,hizi ni karata Sada anacheza na hata nasikia Mwanzele amesema alikuokoa ukitaka kujiua,usiseme Sada amekupush hadi umefika pahali pa kujiua?


Walienda wakalala ukafika usiku wa manane,kila mtu akiwa amelala,kuna gaidi aliingila. Sada amelala,Maria amelala na hata Asiya amelala. Kisha kuna mtu anachongelea chongelea kwa utaratibu sana. Alikuja akachungulia kwa room ya Maria akaona amelala,akakuja kwa room ya Asiya,ndio Asiya amelala,lakini anadumbuliwa na usingizi so hajalala vile sana. Huyu mtu akakuja akasimama kando ya Asiya na bado hatujui ni nani,tunaonyeshwa tu mikono. Kuna kitu huyu mtu anataka kufanyia Asiya but anajishuku na kujirudi. Alikuja akaona kuna karatasi fulani hapo kando ya kitanda,akachukua akaanza kupekua pekua moja baada ya nyingine,kisha akarudisha na akatoka.


Baada ya hapo,huyu huyu mtu akakuja sasa kwa chumba cha Sada. Sada pia ashalala,lakini kando yake,kuna mtu hapo anatafuta kitu. Kwa sasa tushajua ni Major anatafuta ile will yake. Kumbe Sada alishtuka kutoka usingizini hadi akaamka kabisa kabisa akaenda jikoni kujisaidia. Ako na usingizi bado so hajui tofauti ya jikoni na choo so alienda jikoni. Kumbe Major wakati alisikia Sada ameamka,alijificha na wakati Sada alienda jikoni kujisaidia,Major akapata nafasi ya kutoka.


Fatima na yeye,ndio pia anaamka,kuangalia kwenye Major alilala,hakuna mtu,akaanza kumuita akashindwa sana huyu  ameenda wapi. Kumbe Major mwenyewe,wakati Sada anarudi kutoka kwa choo aliona kivuli cha mtu,akajua baasi ninavamiwa. Kuna ile bastola ya Major sada bado ako nayo akaichukua. Kisha akaambia mwenye amejificha huku ndani,utoke ama nikulipue. Asiya aliskia kelele za Sada huko juu akakuja mbio kuona,sasa Sada akingoja kuona mtu,aliona ni Asiya na kumbe Major mwenyewe alikua amejificha nyuma ya kiti na  faster akatoka mbio akafaulu kutoka upande wa nje.


Fatima na yeye alikuja kuona Major ako wapi,akamuona akinyapia nyapia😂😂,ikabidi amwambie wewe toka pole pole watakuona  kwa ule wakati akina Sada,Asiya na Maria wanakimbia sebuleni,hamna mtu. Asiya anauliza Sada,una nini? Sada akasema huku kuna mwizi. Asiya akamwambia una uhakika Sada,kwa sababu pia nimeota ndoto mbaya. Sada alimwambia ndio,kuna mwizi huku  ndani hadi akaendelea kuita akisema kama uko huku ndani,jitokeze,kisha Sada akafyatua risasi kumtishia mwizi eti,mwizi mgani na mtu alishatoka nje akaenda.


Major na Fatima walisikia sauti ya risasi wakajifanya sasa wamekuja mbio kuuliza kuna nini,na ni yeye amekua huku ndani.Sada alikuja bado akiwa na ile bastola yake na Major akamuuliza kuna nini? Sada akamwambia,kuna mtu anajaribu kupima imani yangu na ole wake mwenye amekuja chumbani mwangu anajijua vizuri sana  na namhakikishia hayuko mbali na mbinguni. Fatima alimuuliza,sasa mbona uongee na ukituangalia as if ni sisi,usisahau una maadui kila kona. Sada akamwambia Fatima sikiza,sina adui mimi,adui wangu ni wewe Fatima na huyu Major. Major alimchukua Fatima mkono wakaenda.


Kule mjini kwenye Sultana ako. Sultana akiwa amelala hapa alipewa kachai kwa kikombe na mwenye anamuita mpenzi na tunajua ni JJ sindio? Si JJ, Sultana alishangaa sana wakati alishika mikono za JJ akajua huyu si JJ,wacha sasa aguze guze uso apate wooi huyu si JJ,huyu ni Kokan,makosa. Sultana alianza kupiga nduru lakini Kokan alimwambia relax mum,ama ulidhani sitarudi? Kisha Sultana akaanza kuhisi mikono zake ziko na maji maji akamuuliza mbona nina maji kwa mikoni? Kokan akamwambia hayo si maji,hiyo ni damu na ulidhani nilikufa sio? Sultana alijaribu kuhepa lakini akashikwa na Kokan,ikabidi sasa aweke nduru kubwa hadi JJ akakuja,kumbe ilikua tu ndoto😂


JJ alimuuliza kuna nini Sultana? Sultana akamwambia samahani JJ nimeota ndoto mbaya. JJ akamuuliza ipi hiyo? Sultana hakumwambia,akasema tuachane yu nayo,kwa sasa anasikia njaa. Fatima na yeye alikuja akauliza Major,kwani jana usiku ulikua unajaribu kufanya nini sasa😂Major akamwambia ni mbinu tu nilitaka nipate ile bastola yangu. Fatima alimwambia sikiza,hii niachie mimi I will do my best hii wewe huwezani nayo,lakini Major akamwambia aje,licha ya kuwa sikufaulu, kuna kitu nishapata,theory yenye sikua nayo hapo awali. Theory gani? 

Watch Videos
Search
Search
Recent Updates